Ijumaa, 6 Septemba 2013
USHOGA UMEKITHILI
JESHI la Polisi mkoani Singida
linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika manispaa hiyo kwa
tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja kubwa
baada ya kumnunulia pombe kali aina ya viroba jogoo tisa.Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.
Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.
“Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili apumzike kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla alianguka chini na kisha na kupoteza fahamu,” alisema.
Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile.
Alisema kuwa wasamaria wema walimshuhudia mtuhumiwa akiendelea kufanya unyama huo dhidi ya rafiki yake lakini walipojaribu kumkamata, aliwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.
“Raia wema hao walimbeba muathirika na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye aliweza kupata fahamu ndipo alianza kusikia maumivu makali sehemu yake ya haja kubwa,” alisema.
Alisema muathirika alipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida ambako alibainika kuharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa.
tukio zima la uzinduzi wa song mpya la daimond my number1
EXCLUSIVE PICTURES ZA RED CARPET KWENYE LAUNCHING VIDEO YANGU......MY NUMBER ONE
| Hamis Mwinjuna A.k.a Mwana F.A alikuwepo pia kushow Love.... |
| Interiew zinahusika sana sehemu kama hizi.... |
| Sauda wa Bongo Beats ya Star Tv nae akukosekana ndani ya nyumba..... |
| Chege Chigunda Toka TMK nae alikuwepo..... |
| Flowers awakosekanagi sehemu kama hizi....... wakiongozwa na Number One Diva Hamisa hassani Mobeto. |
| Prince Brother Man Dully Sykes akiwasili ndani ya Nyumba pembeni na FloweR Shadee toka Clouds Tv,presenter wa Cloud 9... |
| Shadee & Dully...Mmmmmh....??? Aya sina usemi |
| Kama kawaida...... |
| Sarah A.k.a Shaa nae ndani |
| Movement zikiendelea na mahojiano mbalimbali kati ya wasanii na presenters wa vituo mbalimbali vya Habari & Blogs kiujumla wakiwa kazini.... |
| Mama yangu Mdogo yanii nikimaanisha Mdogo wake na mama yangu mzazi Bi Sandrah Sammy Asha Baraka,Manager na Owner wa Twanga Pepeta nae alikuwepo... |
| Mwenyewe Naseeb Abdul Nilipowasili,Shuguli ikawa imefikia patamu sasa...... |
| Nikijibu maswali tofauti tofauti toka kwa waandishi wa Habari... |
| Jacquline Wolper toka Bongo Move nae akukosekana..... |
| Jacquline wolper & Qboy Msafii...... |
| My Close friend,Dada yangu Penniel Mungirwa,Presenter wa DTV nae alikuwepo ndani.... |
| Thanks For Coming My bff,close friend,my baby,my everything.... |
| The True Boy Is in the building.... |
| Proffesor Jay a.k.a Father House nae alikuwepo kushow Love kwa mdogo wake..... |
dully anena
DULLY SYKES "NAMFANANISHA DIAMOND NA MAREHEMU KANUMBA KWA UWEZO WA KUTHUBUTU"
Dully Sykes alikuwa akiongea na Bongo5 kwenye uzinduzi wa video ya video mpya ya Diamond uliofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
“Diamond ni namba moja kwasababu yupo tayari kujitoka kwa kila kitu,” alisema Dully. “Naweza kumfananisha Diamond na mtu kama Kanumba. Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.”
Pia Dully amesema mwishoni mwa mwaka huu anatarajia kuiongezea vifaa vipya studio yake ‘4.12’ ili kujiimarisha zaidi kwenye utayarishaji wa muziki ambao anasema kwa sasa anaufurahia zaidi kuliko hata kuimba.
kikwete na kagame kikaoni
BAADA YA BEEF LA CHINI CHINI HATIMAYE KIKWETE AKUTANA NA KAGAME
Baada ya kutolewa ushauri huo, Rais Kagame alionekana wazi kutoukubali, jambo ambalo limezua mambo mengi yakiwamo ya wafanyabiashara wa nchi yake kutangaza kutotumia Bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yao.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu mjini Dar es Salaam jana, ilisema viongozi hao walikutana faragha katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri.
“Viongozi wamekutana kwa saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala.
“Katika mazungumzo hayo, wamekubaliana kuendelea kushirikiana kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo, ilisema viongozi wako nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu, ulioanza jana katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort.
Viongozi wengine ambao wanahudhuria mkutano huo, ni pamoja na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR, Rais wa Sudan Kusini, Silva Kiir, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).
Uhusiano huo, ulizidi kuingia doa baada ya Serikali ya Rwanda kuamua kupandisha ushuru mpya kutoka dola 152 za Marekani hadi dola 500 kwa malori ya Tanzania pekee.
Katika hali ya kushangaza, Serikali ya Rwanda ilisema ushuru huo utatumika kwa kipindi cha wiki moja, jambo ambalo halikukubalika.
Lakini Msemaji wa Umoja wa Wasafirishaji Malori Tanzania (TATOA), Elias Lukumay alisema kuna hatari kubwa ya kupoteza wateja wao kutokana na tozo mpya.
Alisema kama tozo hiyo ikiendelea kutozwa, wafanyabiashara wa malori Tanzania wataathirika kwa kuwa watalazimika kupandisha bei ya usafirishaji karibu dola 500.
WOLPER AVUNJA GLASI YA DIAMOND
Ilikuwa wakati Diamond akisalimiana na mastaa mbalimbali, alipofika kwa Wolper aliigusa kidogo, ikaanguka
Paparazi wetu alipomuuliza Wolper sababu ya glasi hiyo kuvunjika, alijibu: “Hata mimi sijui nini kimetokea, tulikuwa tunasalimiana ghafla tu glasi yake ikadondoka na kupasuka, sijui ni miujiza au nini loh!”
Diamond naye akatia neno: “Nimeshtukia glasi ipo chini tu, daah! Sina hata cha kueleza juu ya hili.”
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)
picha ya mama mzazi wa mmiliki wa ii blog