September
17 2014 mwigizaji Jackline Wolper aliweka kwenye page yake ya Instagram
picha ya mwigizaji mwenzake Lucy Komba alieolewa hivi karibuni na raia
kutoka nje ya Tanzania na kuandika masikitiko yake ya kushindwa
kuhudhuria harusi hii.Wolper aliandika ‘Tukio lililoniuma ni kutohudhuria katika furaha ya milele ya my dada kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu‘ ambapo baada ya post hiyo baadhi ya followers wa Wolper walianza kutukana kwenye comments na kukosoa mavazi ya Maharusi kama unavyoona hapa chini.
Baada
ya matusi kuongezeka ilibidi Wolper aifute hiyo post muda mfupi baadae
na kisha akapost picha yake na kuiambatanisha na haya maneno
>>> ‘Jamani hivi wapenzi wa Insta
tabia ya mimi kuweka picha ya mtu alafu mnakosoa mnatukana sio poa,
kwanini msitukane yangu tuu, naweka picha za maharusi wa watu mnaweza
kuwa Wanamitindo wa kukosoa watu hawajui kuvaa kwanini? sio poa
sijapenda…… haya nibomoeni hapo hiyo picha ni yangu, ruksa‘
Hata
hivyo baadae ya hii post Wolper alipost nyingine ya Maharusi hao lakini
isiyoonyesha sana mavazi yao kwa kiasi kikubwa ambayo ndio hii hapa
chini na kuandika maneno mafupi tu…. ‘One love my sisy’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni