Kupitia You heard ya August 04,Weusi
wamesemekana kucopy wimbo na kuurudia
kuanzia namna wanavyorap mpaka beat
iliyotumika kwenye wimbo huo,Joh Makini
kaongea na kapatikana pia producer wa wimbo
huo NahReel nae kazungumza.
88.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tabora.
Jumanne, 5 Agosti 2014
WEUSI WA COPY NYIMBO
JE WAJUA KUWA #DIAMOND&WEMA WANAONGOZA KWA FOLLOWERS INSTAGRAM
Power couple ya Tanzania, Diamond Platnumz na
Wema Sepetu ndio inayoongoza kwa kuwa na
followers wengi zaidi kwenye mtandao wa
Instagram.
Hii ni orodha kamili (July 31,2014)
1.Diamond Platnumz
183,205
2.Wema Sepetu
168,954
3.Elizabeth ‘Lulu’ Michael
129,047
4.Jokate Mwegelo
102,168
5.Millard Ayo
102,068
6.Jacqueline Wolper
99,545
7. Ommy Dimpoz
95,415
8.Aunty Ezekiel
94,379
9.Kajala
88,769
10.Vanessa Mdee
84,570
11. Shilole
81,904
SINA MUDA WA KUZUNGUMZIA UPUUZI HUO KUUSU RIDHIWANI-RAISI KIKWETE
Taarifa kutoka ofisi ya Rais kuhusu maneno
yanayosemekana kwamba Rais Jakaya Kikwete
kushiriki kusaidia kumwokoa mwanae ambaye ni
mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa
Ridhiwani Kikwete baada ya kukwamatwa na
dawa za kulevya nchini China.Pia office ya raisi imetoa maelezo hayo kupitia hati zionekanazo chini hapa
#DIAMOND_PLATNUM APATA SHAVU JINGINE
Wasanii wa Nigeria wameendelea kumtafuta
Diamond Platnumz kwaajili ya kumshirikisha
kwenye nyimbo zao. Baada ya kushirikishwa na
Waje na Dr Sid, msanii mwingine mkubwa
anayetamba na nyimbo kama ‘Limpopo’ na ‘Pull
Over’ KCEE ameomba kumshirikisha kwenye
wimbo wake mpya.
“Kuna nyimbo nimefanya na KCEE wa ‘Limpopo’
ni nyimbo yake by the way ambayo naenda
kurekodi sasa hivi” Diamond alikiambia kipindi
cha Hitlist cha Choice FM Alhamis iliyopita.
“Nina project nyingi sana hadi naogopa kuzisema
nyingine kwasababu sijaruhusiwa,” aliongeza.
Mshindi huyo wa tuzo 7 za KTMA 2014, aliongeza
kuwa kabla mwaka huu haujaishia, mashabiki
wake wategemee kupata zawadi ya wimbo
aliomshirikisha msanii mkubwa wa Marekani.
“Wategemee pia collabo nyingi sio kutoka Afrika,
kutoka nje ya Afrika kabla ya mwaka haujaisha,”
alisema Diamond japo alikataa kusema ni msanii
gani.
AY asema wanachokifanya WHITEHOUSE
Rapper Ambwene Yessaya ambaye yupo jijini
Washington DC, Marekani pamoja na wasanii
wengine, leo wanatumbuiza mbele ya viongozi
mbalimbali wa Marekani na Africa. Show hiyo
inafanyika kwenye ukumbi wa Newseum mjini
DC
Jana (juzi) ilikuwa ni tour ya kwenda white
house na nini, kuelezewa mambo ya mule ndani
na baadaye usiku tukafanya rehearsal mpaka
usiku wa manane,” AY aliiambia Bongo5 jana.
“Leo (jana) sasa ndo kila kitu, watu tunakutana
kwaajili ya kujadili na baada ya hapo tutafanya
show leo usiku. Chochote kitakachojadiliwa
nitawajuza. Kesho pia ni kuna mkutano
mwingine, pia viongozi mbalimbali marais wako
hapa wanawasili na mwenyeji mkuu yuko hapa,
kesho pia kutakuwa kuna dinner white house,”
alisema.