Hitmaker wa #basi_nenda @MO_MUSIC katika pozi
Ijumaa, 1 Agosti 2014
Jumanne, 29 Julai 2014
NEWS;#bum bum ya #diamond_platnumz inazidi kushika kasi ndani ya #TRACE URBAN
Ni ile video ya #bum bum iliyofanywa na hitmaker wa mdogomdogo @diamond_platnumz akimshirikisha msanii #iyanya kutoka nigeria na video yake iliofanywa na director mkubwa Africa @mr.moe_mussa.Sasa imeanza kushika kasi katika channel ile maarufu ya muziki Africa iitwayo#Trace_tv.Ni hatua nzuri sana kwa muziki wetu wa bongo na congratulation to u @diamond_platnumz fanya ufike mbali zaidi ya hapo
NEWS; Dully Sykes aelezea maana ya wimbo wake ‘Togola’
Dully Sykes ana wimbo mpya uitwayo Togola
uliotengenezwa katika studio zake za 4.12.
Akiongea na EFM hivi karibuni, Dully alidai kuwa
Togola ni salam ya kabila la kizigua.
“Togola maana yake kama salamu tu, kizigua
hicho,” alisema Dully. Unajua mwanaume
unapokuwa mwenyewe huna partner ndani ya
gari inabidi uanze kutizamatizama nikasema
‘mtizame’ lakini kutizamatizama unaweza
kumuona mmoja wapo nje ukashusha kioo
ukasema ‘hello, habari yako, salama’ hapo tayari
ushatogola. Na ndio maana inamaanisha hii
nyimbo kuwa ‘wewe bado ni kijana na unataka
msichana wa maana’, msichana wa maana ni yule
ambaye yupo tayari kuolewa.”
NEWS; Boko Haram wamteka mke wa makamu waziri mkuu wa Cameroon
Wanamgambo wa kundi la Boko Haram,
wamemteka mke wa makamu wa waziri mkuu wa
Cameron, na kuwaua watu watatu baada ya
kuushambulia mji wa kaskazini wa Kolofata.
Wanamgambo hao walivamia makazi ya waziri
Amadou Ali huko Kolofata na kumteka mke wake.
Kiongozi wa dini ambaye pia ni meya wa mji huo
Seini Boukar Lamine naye alitekwa katika
shambulio tofauti.
Boko Haram, kundi la wanamgambo wa kiislamu
la Nigeria limeingia Cameroon hivi karibuni
baada ya nchi hiyo kutuma wanajeshi kuungana
na majeshi ya kimataifa kupambana na
wanamgambo hao.
PICHA; Wema Sepetu aivaa jezi ya Michael Jordan (23), asherehekea Eid na shemejiye, Dimpoz
Wema Sepetu ni shabiki wa mchezaji wa zamani
wa kikapu wa timu ya Chicago Bulls, Michael
Jordan?
Mapenzi yake kwa mchezaji kikapu huyo tajiri,
yameonekana kwenye picha alizopiga wiki hii
(kama sio Jumanne hii) akiwa amevaa jezi
nyeupe ya Chicago Bulls yenye namba 23, namba
aliyokuwa akitumia Jordan. Jezi hiyo imempenza
zaidi Mrs Naseeb baada ya kuisindikiza na tight
yekundu na chini akipigilia sneakers kali.
Wema alikuwa akispend sikukuu ya Eid na
shemeji yake, Ommy Dimpoz aliyekuwa amevaa
kanzu.
NEWS;alichosema #dudubaya kuhusu bifu la allykiba na diamond
Dudubaya anajulikana kama mmoja wa Wasanii
wa siku nyingi bongoflevani ambae pamoja na
headlines zake binafsi huwa anasikika mara
chache akizungumzia au kutoa ushauri kwa ishu
kadhaa za Wasanii wenzake.
Baada ya kusikia yanayoendelea kati ya mastaa
wa bongofleva Diamond na Ally Kiba kwamba
wako kwenye beef, Dudubaya alikutana na
Mimi blogger Dar es salaam na kuyasema yafuatayo >>
‘Wasanii wa Tanzania tuna wapambe na sio
marafiki kwa sababu mpambe unaweza kuwa
umelewa yeye ndio anakoleza ugomvi lakini
rafiki ni yule anaekuonya au kukushauri’
‘Ali Kiba alifanya ngoma na R.Kelly nikafurahia
na nikapenda kinoma kupiga salute kwa mdogo
wangu anakwenda next level, Diamond kaja
kufanya vizuri na ninafurahia… muziki huu
unakosa nguvu kwa sababu ya roho mbaya, wivu
na chuki na kutokuwa makini na
wanaotuzunguka, anakwenda kwa Diamond
anasema hivi kisha anakwenda kwa Ally Kiba
anasema hivi’ – Dudubaya
‘Ninachowashauri hawa wadogo zangu watulie
chini wajitambue ni Wasanii na usanii wao ni
wa kutengeneza pesa, tena watengeneze hata
Tour ya Amani wazunguke nchi nzima..
wazunguke hata Afrika Mashariki na sio hizi
beef’
‘Siku moja nilikua na Dully Sykes na Christian
Bella alafu watu wakawa wanasema Diamond
ooohhh sijui kashindaje tuzo saba, nikawaambia
hivi ukiwa na akili timamu wimbo kama ‘my
number one’ kila kona unayopita, video mpaka
TV za kimataifa zinapiga alafu leo unaweza
video yako ya kijingajinga unategemea
kuishinda ‘my number one’ …….Diamond
alistahili kushinda hizo tuzo saba, mimi sikuona
cha ajabu’
Kwenye sentensi nyingine Dudubaya amesema
‘kuna gazeti moja liliandika eti Diamond
alihonga hela kuchukua hizo tuzo, ni vitu vya
kipumbavu kabisa… hujui kusoma lakini picha
lazima uione, Ali Kiba na Diamond kila mmoja
ana mama yake, wakae chini kama binadamu
wajitambue, waachane na mambo ya watoto wa
hapa mjini hawa ni wapambe tu mwisho wa
siku hawana msaada’
NEWS; Kuhusu simu ya ajabu aliyopokea Tunda Man July 28
Kuna kipindi stori za namba ambazo wengi
walikua wakisema za ajabu na endapo
zikikupigia usipokee zilikuwa zikitawala sana
kwenye mitandao ya kijamii na wengi pia
walikua wakizonyesha namba hizo.
Tunda Man ambaye pia ni miongoni mwa watu
wanaounda kundi la Tip Top Connection Jioni ya
July 28 amepata simu hiyo ambayo amedai
kwake ilikua ni mara ya kwanza kupigiwa kwani
namba hizo hajawahi kuziona zikimpigia kabla
Tunda man ameongea na mimi na
kusema>>’Nilikua nafuturu jana jioni wakati
naendelea kufuturu nikapigiwa simu namba
sikua nazijua kwani zilikua za maajabu
tu,sikupokea,ilipiga kama mara 30 hivi’
‘Baadae nikapokea na kisha nikaiweka mbali
kidogo na mimi wakati nasema hallow ghafla
kitu kama shoti ya umeme kikaanza kutembea
kwenye viganja mpaka kwenye mkono nikakosa
nguvu kabisa nikawaambia jamani nipelekeni
hospital’
‘Tukaenda hospital ya Serikali hapo
Palestina,Dokta akasema huu ugonjwa tangu
ameanza kutibia watu hajakutana nao ni mara
yake ya kwanza hivyo matibabu aliyokuwa
akinipatia ni kama ya mtu aliyepooza ghafla’
‘Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri
ingawa kuna dawa nimepewa zingine nameza
mara 2 kwa siku na vidonge vingine ni mara 3
kwa siku pia nimechomwa sindano’
Hii ndiyo namba iliyompigia Tunda
NEWS: Ushahidi mpya wa Chris Brown kuwa bado ana mapenzi kwa Rihanna
Kila mtu ana story yake ya uhusiano wake na
mpenzi wake lakini hii story ya Chris Brown na
Rihanna inachukua attention ya watu wengi
kutokana na mambo yanayoendelea kati yao.
Kila muda ukipita inatokea tetesi kwamba Chris
Brown ana mawasiliano ya siri na Rihanna lakini
bado hakukuwa na ushahidi kuthibitisha hilo.
Kitu kipya hivi sasa kinachotafsiriwa kwamba
bado Chris ana mawazo na kumbukumbu juu ya
uhusiano wake na Rihanna ni kutokana na
picha ya rafiki wa Rihanna. Melissa Ford ambaye
ni rafiki wa karibu wa Rihanna ali post picha ya
Chris na Rihanna na kuandika kuwa ni hao ndio
couples anaowapenda.
Baada ya hapo Chris Brown ali like hiyo picha
na kuonyesha kwamba amefurahia hiyo post.
Kutokana na ukaribu wa Rihanna na Melissa sio
rahisi kwa Melisa ku post picha hiyo kama
mambo bado ni mabaya kati ya Riri na Chris.
Kama kuna lolote linaendelea kati ya Chris
Brown na Rihanna lazima Melissa Ford awe
anajua kwasababu wapo karibu sana.
Wachambuzi wanasema kwamba kuna kitu
kinaendelea chini kwa chini kati ya Chris Brown
na Rihanna na hivi karibuni kinaweza kuwekwa
wazi.
NEWS: Shakira ni mjamzito tena? Hiki alichokisema Gerard Pique
Kwa mara nyingine tena familia ya mwanamuziki
maarufu duniani Shakira na mchumba wake
mwanasoka, Gerard Pique - imeingia kwenye
‘headlines’ za vyombo vya haari ulimwenguni.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ukiwemo
mtandao wa tracetv unaripoti kwamba
mchumba wa Shakira, Gerard Pique amekaririwa
akisema hitmaker wa ‘Hips Dont Lie’ ni
mjamzito kwa mara nyingine tena.
Kulikuwepo na tetesi nyingi hasa baada ya
Shakira kutumbuiza kwenye kombe la dunia
liloisha hivi karibuni nchini Brazil, lakini kambi
ya Shakira ilikanusha uvumi huo.
Lakini jana kupitia channel ya kilatino ya “Fox
News” – kituo hicho cha TV kiliripoti kwamba
Pique amewathibishia kwamba Shakira ni
mjamzito.
Pique na Shakira tayari wana mtoto mmoja wa
kiume waliyempa jina la Milan, ambaye alizaliwa
mnamo mwaka 2012, miaka miwili baada ya
wazazi wake kuanza mahusiano yao wakati wa
utengenezwaji wa wimbo wa kombe la dunia
2010.
NEWS:Nicki Minaj anamiliki headlines kwenye internet na hizi picha
Ikifika tarehe tarehe 4 mwezi wa 8 mashabiki
wote wa Nicki Minaj watafungua iTunes
kununua wimbo mpya wa Nick Minaj unaitwa
Anaconda. Lakini hivi sasa kick kubwa ni cover
ya picha za wimbo huo ambayo alipost kwenye
instagram na hadi hivi sasa imepata likes zaidi
ya milioni 3.
Picha ya kwanza imepigwa kutoka kwa nyuma na
hivi sasa ametoa nyingine iliyopigwa kutoka
mbele.
Jumapili, 27 Julai 2014
POST ZA MASTAA WETU WA BONGO #INSTAGRAM
Instagram
ni mtandao mwingine wa kijamii unaozidi kupata Wanachama wapya kila
siku kutokana na aina yake ya kupost pichaz ambapo umekua ukitumiwa sana
hata na watu maarufu na kurahisisha kazi ya kusambaza habari kama
unavyoona baadhi ya mastaa kwenye hii post.
MJ Records imepata studio mpya? amepost hii picha C.E.O mwenyewe Master J na kuandika haya maneno hapa chini…
******************************
Mwigizaji Kajala baada ya kuweka hii picha akaandika ‘Mtu anapokwambia huwezi kufanya kitu flani usiache kukifanya, tabasamu na kusema nitakuonyesha’
******************************
Staa wa bongoflevani Nay wa Mitego yuko nchini Kenya kufanya video yake mpya ambayo ameshea moja ya picha ya utengenezwaji wake kama unavyoona hapa chini…


******************************
Saa kadhaa baada ya kusambaza single zake mbili mpya kwenye Radio Stations mbalimbali Tanzania, mwimbaji Ali Kiba amepost hii kwenye instagram na kuambatanisha na hiyo caption chini yake.


******************************
Ifuatayo ni TBT ya CMB Prezzo kutoka Kenya.


******************************
Jokate yuko nchini Kenya ambako kwa July 25 pekee ameonekana akihojiwa kwenye vyombo viwili vya habari kama alivyopost hapa chini akiwa na Mtangazaji William Tuva wa Citizen TV/Radio.




******************************
Hapa chini ni meneja wa kundi la Tiptop Connection ambae pia ni meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale ambae ameshafika Marekani na Diamond kuhudhuria tuzo za AFRIMMA.

******************************Ni halali yako kupata kila kinachonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB
#NEWS: Mtangazaji wa 102.5 Choice FM kuiwakilisha Tanzania kwenye kongamano la Obama
Kabae ataungana na Waandishi wengine zaidi ya 20 kutoka nchi mbalimbali Afrika kwenye tour Washington DC na kwenye jiji la Atlanta kwa ajili ya U.S – African Leaders Summit and Young African Leadership Initiative (YALI) Forum hosted by President Obama.
These two initiatives build on, and seek to further strengthen partnership between United States and Sub-Saharan Africa in strengthening democratic institutions, accelerating economic growth, promoting trade and investments, advancing peace and security and investing in the next generation of African leaders. For more information about the events visit.
WAIMBAJI WA INJILI AKIWEMO #BAHATI BUKUKU WAPATA AJALI
MATOKEO YA TUZO ZA #AFRIMMA 2014 AMBAZO #DIAMOND.. ALIKUWA AKIWANIA
Zinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news za ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja Babu Tale ambae nae kahudhuria tuzo hizi Marekani alienitumia msg kwa kusema wametangaza ukumbini kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.

Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
Lady
Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua
anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya,
Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.Producer bora wa mwaka ni Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana Dj Oskido wa South Africa, Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
Stori zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo endelea kukaa karibu na millardayo.com mtu wangu ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili ambalo limewahusisha wakali wengine kama Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour, Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.
Ni halali yako kupata kila kinachonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa
