Jumanne, 5 Agosti 2014

#DIAMOND_PLATNUM APATA SHAVU JINGINE

Wasanii wa Nigeria wameendelea kumtafuta
Diamond Platnumz kwaajili ya kumshirikisha
kwenye nyimbo zao. Baada ya kushirikishwa na
Waje na Dr Sid, msanii mwingine mkubwa
anayetamba na nyimbo kama ‘Limpopo’ na ‘Pull
Over’ KCEE ameomba kumshirikisha kwenye
wimbo wake mpya.
“Kuna nyimbo nimefanya na KCEE wa ‘Limpopo’
ni nyimbo yake by the way ambayo naenda
kurekodi sasa hivi” Diamond alikiambia kipindi
cha Hitlist cha Choice FM Alhamis iliyopita.
“Nina project nyingi sana hadi naogopa kuzisema
nyingine kwasababu sijaruhusiwa,” aliongeza.
Mshindi huyo wa tuzo 7 za KTMA 2014, aliongeza
kuwa kabla mwaka huu haujaishia, mashabiki
wake wategemee kupata zawadi ya wimbo
aliomshirikisha msanii mkubwa wa Marekani.
“Wategemee pia collabo nyingi sio kutoka Afrika,
kutoka nje ya Afrika kabla ya mwaka haujaisha,”
alisema Diamond japo alikataa kusema ni msanii
gani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni