Miili ikiwa imefungwa kwenye mifuko na kutupwa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
Chama cha Madaktari nchini Tanzania kimelaani kitendo
cha kutupwa kwa viungo vya binadamu nje ya jiji la Dar es Salaam
kinyume cha sheria.
Rais wa chama hicho, Dk. Primus Saidia ametaka hatua madhubuti
zichukuliwe dhidi ya wahusika ikiwemo kupigwa marufuku kwa mtu au
taasisi iliyohusika kuendesha shughuli zozote za utafiti kwa kutumia
viungo vya binadamu.Dk Primus ameweka bayana kwamba, licha ya fani hiyo ya udaktari kuruhusiwa kutumia viungo vya binadamu katika shughuli mbali mbali za utafiti kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kimaifa lakini ameelezea kwamba kitendo hicho kimekiuka haki za binadamu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho cha Madaktari hapa jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo ametaka hatua madhubuti zikuchuliwe dhidi ya wahusika ikiwemo kufungiwa.
Sakata la kutupwa kwa viungo hivyo kinyume cha sheria katika mji wa Mbweni nje ya jiji la Dar es Salaam siku mbili zilizopita, lilizua taharuki miongoni mwa watu wa kada mbalimbali.
Tayari watu wanane kutoka chuo cha udaktari cha IMTU kilichopo hapa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusishwa kwa kutupwa kwa viungo hivyo ambavyo viliwekwa katika mifuko ya plastiki ipatayo 85.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni