
Mkali wa kuchekesha na sanaa za
majukwaani Afrika Mashariki, Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani
kali hapo August 2, katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo
linaloandaliwa na kituo cha Radio 5 litaambatana na burudani ya muziki
kutoka ODAMA Band, pamoja na mchekeshaji Fredi Omondi kutoka Kenya na
Pilipili wa Tanzania.
Akizungumzia tukio hilo
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis alisema kuwa
wameamua kumualika Kansiime kwa sababu ana kipaji cha hali ya juu katika
uchekeshaji na ana mashabiki wengi Tanzania.
“Kansiime ni mchekeshaji ambaye
amejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa uwezo wake wa kuweka
utani kwenye maisha ya kawaida’ alisema Francis.
Kansiime amejipatia umaarufu kupitia
mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video
akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali
za maisha.
Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia
huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha
Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda
na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Burudani hii ya Kansiime, ambayo
itakwenda kwa jina la Cheka Kwa Nguvu, itaanza saa moja usiku na tiketi
zitauzwa shilingi elfu 90,000 kwa mtu mmoja, na shilingi 700,000 kwa
meza ya watu nane.
‘Kama ambavyo mwandishi wa vitabu, Maya
Angelou alivyowahi kusema, “Simwamini mtu yeyote asiye cheka” tukio hili
linalenga kuonesha umuhimu wa kucheka katika maisha yetu ya kila siku”
alihitimisha Francis.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni