Jumanne, 29 Julai 2014

NEWS; Boko Haram wamteka mke wa makamu waziri mkuu wa Cameroon

Wanamgambo wa kundi la Boko Haram,
wamemteka mke wa makamu wa waziri mkuu wa
Cameron, na kuwaua watu watatu baada ya
kuushambulia mji wa kaskazini wa Kolofata.
Wanamgambo hao walivamia makazi ya waziri
Amadou Ali huko Kolofata na kumteka mke wake.
Kiongozi wa dini ambaye pia ni meya wa mji huo
Seini Boukar Lamine naye alitekwa katika
shambulio tofauti.
Boko Haram, kundi la wanamgambo wa kiislamu
la Nigeria limeingia Cameroon hivi karibuni
baada ya nchi hiyo kutuma wanajeshi kuungana
na majeshi ya kimataifa kupambana na
wanamgambo hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni