Jumanne, 29 Julai 2014

NEWS: Ushahidi mpya wa Chris Brown kuwa bado ana mapenzi kwa Rihanna

Kila mtu ana story yake ya uhusiano wake na
mpenzi wake lakini hii story ya Chris Brown na
Rihanna inachukua attention ya watu wengi
kutokana na mambo yanayoendelea kati yao.
Kila muda ukipita inatokea tetesi kwamba Chris
Brown ana mawasiliano ya siri na Rihanna lakini
bado hakukuwa na ushahidi kuthibitisha hilo.
Kitu kipya hivi sasa kinachotafsiriwa kwamba
bado Chris ana mawazo na kumbukumbu juu ya
uhusiano wake na Rihanna ni kutokana na
picha ya rafiki wa Rihanna. Melissa Ford ambaye
ni rafiki wa karibu wa Rihanna ali post picha ya
Chris na Rihanna na kuandika kuwa ni hao ndio
couples anaowapenda.
Baada ya hapo Chris Brown ali like hiyo picha
na kuonyesha kwamba amefurahia hiyo post.
Kutokana na ukaribu wa Rihanna na Melissa sio
rahisi kwa Melisa ku post picha hiyo kama
mambo bado ni mabaya kati ya Riri na Chris.
Kama kuna lolote linaendelea kati ya Chris
Brown na Rihanna lazima Melissa Ford awe
anajua kwasababu wapo karibu sana.
Wachambuzi wanasema kwamba kuna kitu
kinaendelea chini kwa chini kati ya Chris Brown
na Rihanna na hivi karibuni kinaweza kuwekwa
wazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni