Jumanne, 29 Julai 2014

NEWS;alichosema #dudubaya kuhusu bifu la allykiba na diamond

Dudubaya anajulikana kama mmoja wa Wasanii
wa siku nyingi bongoflevani ambae pamoja na
headlines zake binafsi huwa anasikika mara
chache akizungumzia au kutoa ushauri kwa ishu
kadhaa za Wasanii wenzake.
Baada ya kusikia yanayoendelea kati ya mastaa
wa bongofleva Diamond na Ally Kiba kwamba
wako kwenye beef, Dudubaya alikutana na
Mimi blogger Dar es salaam na kuyasema yafuatayo >>
‘Wasanii wa Tanzania tuna wapambe na sio
marafiki kwa sababu mpambe unaweza kuwa
umelewa yeye ndio anakoleza ugomvi lakini
rafiki ni yule anaekuonya au kukushauri’
‘Ali Kiba alifanya ngoma na R.Kelly nikafurahia
na nikapenda kinoma kupiga salute kwa mdogo
wangu anakwenda next level, Diamond kaja
kufanya vizuri na ninafurahia… muziki huu
unakosa nguvu kwa sababu ya roho mbaya, wivu
na chuki na kutokuwa makini na
wanaotuzunguka, anakwenda kwa Diamond
anasema hivi kisha anakwenda kwa Ally Kiba
anasema hivi’ – Dudubaya
‘Ninachowashauri hawa wadogo zangu watulie
chini wajitambue ni Wasanii na usanii wao ni
wa kutengeneza pesa, tena watengeneze hata
Tour ya Amani wazunguke nchi nzima..
wazunguke hata Afrika Mashariki na sio hizi
beef’
‘Siku moja nilikua na Dully Sykes na Christian
Bella alafu watu wakawa wanasema Diamond
ooohhh sijui kashindaje tuzo saba, nikawaambia
hivi ukiwa na akili timamu wimbo kama ‘my
number one’ kila kona unayopita, video mpaka
TV za kimataifa zinapiga alafu leo unaweza
video yako ya kijingajinga unategemea
kuishinda ‘my number one’ …….Diamond
alistahili kushinda hizo tuzo saba, mimi sikuona
cha ajabu’
Kwenye sentensi nyingine Dudubaya amesema
‘kuna gazeti moja liliandika eti Diamond
alihonga hela kuchukua hizo tuzo, ni vitu vya
kipumbavu kabisa… hujui kusoma lakini picha
lazima uione, Ali Kiba na Diamond kila mmoja
ana mama yake, wakae chini kama binadamu
wajitambue, waachane na mambo ya watoto wa
hapa mjini hawa ni wapambe tu mwisho wa
siku hawana msaada’

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni