Kuna kipindi stori za namba ambazo wengi
walikua wakisema za ajabu na endapo
zikikupigia usipokee zilikuwa zikitawala sana
kwenye mitandao ya kijamii na wengi pia
walikua wakizonyesha namba hizo.
Tunda Man ambaye pia ni miongoni mwa watu
wanaounda kundi la Tip Top Connection Jioni ya
July 28 amepata simu hiyo ambayo amedai
kwake ilikua ni mara ya kwanza kupigiwa kwani
namba hizo hajawahi kuziona zikimpigia kabla
Tunda man ameongea na mimi na
kusema>>’Nilikua nafuturu jana jioni wakati
naendelea kufuturu nikapigiwa simu namba
sikua nazijua kwani zilikua za maajabu
tu,sikupokea,ilipiga kama mara 30 hivi’
‘Baadae nikapokea na kisha nikaiweka mbali
kidogo na mimi wakati nasema hallow ghafla
kitu kama shoti ya umeme kikaanza kutembea
kwenye viganja mpaka kwenye mkono nikakosa
nguvu kabisa nikawaambia jamani nipelekeni
hospital’
‘Tukaenda hospital ya Serikali hapo
Palestina,Dokta akasema huu ugonjwa tangu
ameanza kutibia watu hajakutana nao ni mara
yake ya kwanza hivyo matibabu aliyokuwa
akinipatia ni kama ya mtu aliyepooza ghafla’
‘Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri
ingawa kuna dawa nimepewa zingine nameza
mara 2 kwa siku na vidonge vingine ni mara 3
kwa siku pia nimechomwa sindano’
Hii ndiyo namba iliyompigia Tunda
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni