Jumanne, 29 Julai 2014

NEWS: Shakira ni mjamzito tena? Hiki alichokisema Gerard Pique

Kwa mara nyingine tena familia ya mwanamuziki
maarufu duniani Shakira na mchumba wake
mwanasoka, Gerard Pique  - imeingia kwenye
‘headlines’ za vyombo vya haari ulimwenguni.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ukiwemo
mtandao wa tracetv unaripoti kwamba
mchumba wa Shakira, Gerard Pique amekaririwa
akisema hitmaker wa ‘Hips Dont Lie’ ni
mjamzito kwa mara nyingine tena.
Kulikuwepo na tetesi nyingi hasa baada ya
Shakira kutumbuiza kwenye kombe la dunia
liloisha hivi karibuni nchini Brazil, lakini kambi
ya Shakira ilikanusha uvumi huo.
Lakini jana kupitia channel ya kilatino ya “Fox
News” – kituo hicho cha TV kiliripoti kwamba
Pique amewathibishia kwamba Shakira ni
mjamzito.
Pique na Shakira tayari wana mtoto mmoja wa
kiume waliyempa jina la Milan, ambaye alizaliwa
mnamo mwaka 2012, miaka miwili baada ya
wazazi wake kuanza mahusiano yao wakati wa
utengenezwaji wa wimbo wa kombe la dunia
2010.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni